Wednesday, March 11, 2015

SOMA HUKUMU WALIYOPEWA PHARELL NA ROBIN THICKLE BAADA YA KUPATWA NA HATIA YA KU- COPY WIMBO BLURRED LINES

Katika zama tunazoishi hususani za tekinolojia inayokua kwa kasi namna hii, masuala ya haki miliki yanaendelea kuwa changamoto ya kidunia. Mfano ni uamuzi wa mahakama huko Los Angeles uliotolewa hivi katika kesi iliyokuwa imefunguliwa na familia ya Marehemu Marvin Gaye ambaye alikuwa miongoni mwa wanamuziki mahiri sana enzi zake.
Familia ilikuwa inawatuhusu wanamuziki Pharrell Williams na Robin Thicke kwamba wimbo wao wa mwaka 2013 uliotamba vilivyo wenye jina “Blurred Lines”, sio wao bali waliiga takribani midundo nk kutoka katika nyimbo ya baba yao ya mwaka 1977 iliyoitwa “Got to Give It Up”.

Katika taarifa ambazo zimeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani, mahakama hiyo imeridhia mashtaka yaliyowasilishwa na kukubali kwamba ni kweli Pharrell na Robin Thicke walifanya “uhuni” na hivyo kuwaagiza wawalipe familia ya Marvin Gaye kiasi cha Dola Za Kimarekani $7.3 (zaidi ya Bil. 126 Tshs). Hata hivyo mwanamuziki mwingine ambaye alishirikishwa katika wimbo huo, T.I mahakama imeona hana hatia yoyote na hivyo hahusiki katika malipo.
Tayari wakili aliyekuwa akiiiwakilisha familia ya Marvin Gaye ameshapeleka maombi ya kusimamisha uuzwaji wowote wa “Blurred Lines”. Hata hivyo kiwango cha Dola Za Kimarekani Milioni $7.3 ni kidogo kulinganisha na kile ilichokuwa inataka kulipwa familia ya Marvin Gaye cha dola milioni $45.

BONYEZA HAPA KUANGALIA JINSI NYIMBO HIZO ZINAVYOSHABIHIANA.

No comments:

Post a Comment