Tukio la ajali mbaya kati ya treni la shirika la reli tanzania lililokuwa linaelekea kuchkua mabehewa na Roli la mizigo ( lenye usajili T535 CCT) la kampuni ya Coast Millers Limited ambao ni watengenezaji wa unga wa ngano wa nyati limeripotiwa kutokea leo maeneo ya chang'ombe dar es salaam jirani na machinga complex. tukio hilo limejiri leo march 27,2015 saa 12 hasubuhi ambapo gari hilo lilikuwa likipita kwa kasi kuwahi kuvuka reli hiyo kabla ya foleni na ndipo lilipolutan na treni hiyo.
ASKARI WAKITAZAMA AJALI HIYO.(PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS)
Akizungumza na mwandishi wa habari, Ofisa Oparesheni Shirika la Reli,
Mohamed Kanka, alisema kuwa treni hiyo ilikuwa ikipita majira ya saa
kumi na mbili alfajiri na kugongwa na gari iliyokuwa ikipita pasipo
dereva wa gari hiyo kuzingatia alama iliyokuwa ikionesha kama sehemu
hiyo kuna reli.
Alisema kuwa katika ajali hiyo dereva wa gari na dereva aliyekuwa
katika treni hiyo wameumia na wamekimbizwa Hospitali ya Amana Ilala kwa
ajili ya kupatiwa matibabu.
Vilevile alisema baada ya ajali hiyo kutokea gari jingine lililokuwa
limesimama liligongwa na kichwa cha treni baada ya kuiacha njia yake na
kuelekea upande wa magari yaliyokuwa yakipita.
Ofisa huyo amewaasa madereva kuwa makini wanapofika eneo lenye alama
kuonyesha mbele kuna reli kwani ajali nyingi hutokea kutokana na
madereva wasiokuwa waangalifu.
UMATI WA WATU UKISHUHUDIA AJALI HIYO (PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS)
ENDELA KUPITIA tegeinc.blogspot .com KWA HABARI MBALI MBALI ZA KIUCHUMI,KITAIFA,KIMATAIFA NA BURUDANI.
No comments:
Post a Comment