Mechi no.117 iliyowakutanisha Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa,
imeingiza jumla ya sh. milioni 436,756,000 kutokana na idadi ya
watazamaji 49,758 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
Watazamaji
309 walikata tiketi za VIP A,
1,310 VIP B,
1,533 VIP C,
Rangi ya
Machungwa (Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani wakiingia
watazamaji 36,693.
Mgawanyo wa mapato ya mchezo huo ni
VAT 18%
sh.66,623.796, FDF timu mwenyeji sh. 17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700,
Gharama za tiketi sh.11,669,600.
Mgao wa Uwanja sh.
50,037,540.51, Gharama za mchezo sh.28,354,606.29, Bodi ya Ligi (TPLB)
sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20, DRFA sh. 11,675,426.12, klabu
ya Simba sh. 115,086,343 huku Yanga wakipata sh.81,727.83.
Wakati
huo huo Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea kesho siku ya jumanne katika
uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro
watawakaribisha Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani.
Siku
ya jumatano JKT Ruvu watawakaribisha Young Africans katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa
wenyeji wa timu ya Azam FC.
Aidha mechi ya Kombe la Shirikisho
(CC) barani Afrika kati ya Young Africans dhidi ya timu ya FC Platinum
ya Zimbabwe, itafanyika siku ya jumapili Machi 15, 2015 katika Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Wednesday, March 11, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment