Wednesday, March 25, 2015

PAZIA LA TUZO ZA MUZIKI ZA KILIMANJARO (KTMA 2015) LAFUNGULIWA RASMI

Msimu mpya wa tuzo za muziki Tanzania zijulikanazo kama Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kwa mwaka 2015 umefunguliwa rasmi.
akizindua msimu huo katika ukumbi wa LAPF uliopo barabara ya ally hassan mwinyi, meneja wa bia ya kilimanjaro bi PAMELA KIKULI alisema “Kilimanjaro Premium Lager ni bia ya watanzania na imejikita katika kuwaletea burudani na pia kutoa majukwaa ambayo yanawapa Watanzania fursa ya kukuza vipaji mbalimbali.. hii tumeithibitisha kwa juhudi za makusudi za kutenga fungu kubwa na kuongeza ushiriki wa wataalaam mbali mbali kwenye fani husika ili kuziendeleza, kuzikuza na kuziongezea thamani tuzo hizi mwaka hadi mwaka sambamba na umaarufu kuongezeka kwenye medani za Kimataifa.”
Bia ya kilimanjaro ambayo ni mdhamini mkuu wa tuzo hizo kwa mwaka huu imedhamini tuzo hizo kwa kiasi cha takribani bil 1.1 za kitanzania kuhakikisha tuzo za mwaka huu zinafanyika kwa ubora na ufanisi wa kimataifa.
Meneja huyo aliongeza kuwa msimu huu hautakuwa na mabadiliko katika vipengele au mfumo wa kuwapata wateule ila kutakuwa na maboresho makubwa katika mfumo wa upigaji kura ili kuongeza ufanisi.

Kura za maoni zitaanza kupigwa tarehe March 30 ambapo shabiki ataweza kupendekeza nani ama nyimbo zipi ziwemo kwenye vipengele vyote vya KTMA 2015.
Watu watapiga kura kupitia mtandao, Whatsapp na SMS na utaratibu uliopo ni kwamba namba moja ya simu itatumika kupiga kura moja kwenye kila kipengele.
Hizi ni njia ambazo utazitumia kupiga kura;
  1. Whatsapp – 0686 528 813.
  2. SMS – 15415.
  3. Mtandao – www.ktma.co.tz
BASATA wamesisitiza usimamizi mzuri wa nyimbo zinazoingizwa; “Kama kuna wimbo ulifungiwa na BASATA hautaruhusiwa kushiriki kwenye mchakato“– BASATA.

No comments:

Post a Comment