Watu
zaidi ya 30 wanasadikiwa kupoteza na maisha na wengine kadhaa
kujeruhiwa vibaya sana katika ajali mbaya iliyotokea mapema leo
asubuhi,maeneo ya Changarawe,Mafinga
Mkoani Iringa,iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni
ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es
salaam.
Ajali
hiyo imetokea baada ya Lori hilo la Mizigo lililokuwa likitokea Jijini
Dar kuelekea Mbeya kuligonga na kuliangukia basi hilo wakati lililokuwa
likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara wakati wakiwa kwenye
mwendo walipokuwa wakipishana.
Hali
ya Uokoaji wa maiti na majeruhi walionasa kwenye ajali hiyo bado ni
tete na hasa kutokana na ukosefu wa Gesi ya kukata basi hilo kukosekana
eneo lote la Mafinga,Juhudi zinafanyika ili kuweza kuokoa majeruhi pamoja na maiti.
Blog ya tege inc inatoa pole kwa wahanga wote na wafiwa wote kutokana na ajali iyo. Mungu azipokee na kuzilaza mahala pema peponi roho za marehemu wote katika ajali hii na awajaalie kupona kwa haraka majeruhi wote.
Amin.
No comments:
Post a Comment