Wednesday, April 1, 2015

VIPAJI WILAYA YA KINONDONI SASA KUNG'AMULIWA, KUENDELEZWA.


Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, katika kuhakikisha anainua vipaji ya watoto na vijana  kutoka wilayani mwake ameamua kuanzisha Shindano la Kinondoni Talent Search, ambayo litahusika na kusaka vipaji vya watoto na vijana wenye vipaji vya kucheza, kuimba, kuchekesha na vinginevyo kutoka wilaya kinondoni.
Akizungumza na wakati wa uzinduzi huo, mh Makonda amesema lengo  kubwa la tamasha hilo lenye kauli mbiu ya “Kipaji chako, ajira yako”  litakuwa ni  kuwatafuta na kuwaendeleza vijana wenye vipaji mbalimbali vikiwemo kuimba, kucheza na kuchekesha waliokosa nafasi ya kusikika kutokana na hali ya uchumi kuwa mgumu.
Mh, Paul Makonda akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Kinondoni Talents Search
“Shindano litaanza hivi karibuni, tunataka tuwawezeshe vijana kutoka Wilaya ya Kinondoni waweze kujiajiri kupitia vipaji vyao, na  ili kuhakikisha shindano linaenda vizuri tumeandaa kamati ya watu watano ambao kwa namna moja au nyengine wanatokea kwenye tasnia hiyo ya sanaa wakiwemo Jokate Mwegelo, Mc Pilipili na Peter Msechu,” alisema Makonda,
Msanii Peter Msechu akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.
Akizungumza na waandishi, amesema kuwa Kinondoni Talent Search, ni mpango utakaolenga kuwatambua na kuwaendeleza vijana waishio kwenye wilaya ya Kinondoni, wenye vipaji vya kuimba, kuchekesha na kucheza  ambao wengi wao wapo katika mazingira magumu ya kiuchumi jambo linalowafanya kushindwa kuonesha vipaji vyao.
Amesema kutokana watoto hao wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kuishi katika maisha magumu na kusema kuwa lengo kuu la mpango huu ni kuwawezesha kupata njia za kutimiza ndoto zao kupitia vipaji vyao kwa kuwatafutia nafasi za mafanikio kutokana na ukuaji wa sanaa, kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na wadau muhimu kwenye sekta yao.
Mc pilipili akitoa maelezo wakati wa uzinduzi (picha kwa hisani ya Global publ)
Blogu hii na tasnia ya habari kwa ujumla, inatambua na inampongeza sana mh Paul Makonda kwa hatua nzuri ya kuamua kuendeleza vipaji ambavyo vingi vinapotea sababu ya kukosa wadau wa kuviendeleza. Kwa pamoja tunaunga mkono harakati hizi za ukombozi dhidi ya vijana wenzetu ili kuvifanya vipaji vya vijana wenzetu kuwa ajira itakayotumika kusaidia na kukomboa jamii yote inayotuzunguka. Tunaahidi kuwa nawe bega kwa bega kutimiza jukumu hili zito.
- Tege inc blog -

Friday, March 27, 2015

USHIRIKIANO! KAGAME AMWAGIA SIFA KIKWETE.






Rais wa Tanzania mh Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa kenya mh Paul kagame wakiteta jambo wakati wa mkutano uliwakutanisha wakuu wa nchi wa ukanda wa kati, Dar es salaam Tanzania.

Dar es Salaam. Rais wa Rwanda, Paul Kagame amemwagia sifa Rais Jakaya Kikwete kwa kuboresha huduma za Bandari ya Dar es Salaam na kuwezesha mizigo inayosafirishwa kwenda Rwanda kufika mapema zaidi kuliko ilivyokuwa miaka michache iliyopita.
Akizungumza kwa furaha wakati marais hao walipotembelea kitengo cha kushusha na kupakia mizigo cha TICTS bandarini hapo jana, Rais Kagame alisema hatua iliyopigwa ni mafanikio kwa Rwanda.
Napenda nimpongeze Rais Kikwete kwa mafanikio yaliyopatikana bandarini, kazi ikiwa nzuri (bandarini Dar), huko kwetu Rwanda tunafaidika,” alisema Rais Kagame. Alisema Rwanda itaendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufaika kibiashara.
Rais Kikwete alisema tangu ameingia madarakani, ameitembelea Bandari ya Dar es Salaam mara nne, lakini ziara tatu za mwanzo hazikuwa za furaha kutokana na wizi, ucheleweshaji wa mizigo na malalamiko yaliyokuwa yamekithiri bandarini hapo.
Huku akionekana mwenye furaha, Rais Kikwete alisema Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inatakiwa ipongezwe kwa kufanikiwa kuwaondoa wezi waliokuwa wakiirudisha nyuma.
“Kwa hiyo kusikia habari nzuri zinazofanywa hapa mnanifurahisha sana. Kulikuwa na genge la wezi, sifa mbaya, meli zinakaa siku 23, mambo ya ajabu sana, leo meli zinakaa kwa muda mfupi na hakuna udokozi, kumbe mnaweza kuwa waaminifu,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa kutokana na uhalifu uliokuwa unafanyika bandarini hapo, Burundi nayo ilikuwa ikiilalamikia Tanzania.
“Burundi walilalamika mambo tunayowafanyia, lakini ukiwaangalia ni kama vile wanamlaumu Mungu kwa nini aliiweka Tanzania katikati yao na bahari, pengine ingekuwa nchi nyingine ingewafanyia tofauti,” alisema Rais Kikwete.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPA, Awadhi Massawe alisema tangu kufanyika kwa maboresho bandarini hapo, idadi ya mizigo inayopelekwa katika nchi za Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda imeongezeka.
Mkurugenzi Mtendaji wa TICTS, Walles Paul alisema pamoja na kitengo hicho kuboresha utoaji wa huduma zake, bado kinakabiliwa na changamoto ya eneo la kufanyia kazi.
“Nafasi haitoshi tunahitaji kuongezewa ili tusirudi nyuma tulikotoka,” alisema Paul.
Mapema jana asubuhi katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa wawekezaji, Rais Kagame alisema ili kuendana na kasi ya ukuaji wa uchumi, ni muhimu kuhakikisha miundombinu ya uchukuzi hasa reli inaboreshwa.

NDONGA! BONDIA MOHAMMED MATUMLA,MCHINA KUZICHAPA LEO DIAMOND JUBILEE KUWANIA MKANDA WA UBINGWA WA DUNIA.

Pambano kali la masumbwi la kugombea taji la ubingwa wa dunia wa WBF la uzito wa bantam (raundi 12) kati ya bondia MOHAMMED MATUMLA kutoka Tanzania na bondia WANG XIN HUA kutoka china  linatarajiwa kuafanyika leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee dar es laam Tanzania.
Bondi WANG XIN HUA akitunishiana misuli na bondia MOHAMMED MATUMLA wakatia wa kupima uzito mapema leo.

          Akizungumza na mwandishi wetu wa habari,promota wa pambano hilo Jay Msangi "jiwe gumu" alisema kuwa maandalizi yote ya pambano hilo yamekamilika na pambano litasimamiwa na raisi wa shirikisho la ngumi WBF ambaye amewasili siku kadhaa zilizopita. Pia pambano hilo litashuhudiwa na bingwa wa zamani wa mchezo huo wa uzito wa juu FRANCIS BOTHA ambaye amewasili siku kadhaa zilizopita.


Mbali na pambano hilo la Matumla na Wang xin hua, mapambano kadhaa ya utangulizi yatahusisha mabondia wa Tanzania wenye upinzani.
 JAPHET KASEBA VS MADA MAUGO 
 
MFAUME MFAUME VS COSMAS CHEKA
Pia,bondia Thomas mashali atapanda ulingoni kuonyeshana ubabe na Karama nyilawila.

MSIMAMO WA BEI YA MADAFU LEO IJUMAA 27/03/2015


NEWS: AJALI YA TRENI NA GARI DAR ES SALAAM LEO

        Tukio la ajali mbaya kati ya treni  la shirika la reli tanzania lililokuwa linaelekea kuchkua mabehewa na Roli  la mizigo ( lenye usajili T535 CCT) la kampuni ya Coast Millers Limited ambao ni watengenezaji wa unga wa ngano wa nyati limeripotiwa kutokea leo maeneo ya chang'ombe dar es salaam jirani na machinga complex. tukio hilo limejiri leo march 27,2015 saa 12 hasubuhi ambapo gari hilo lilikuwa likipita kwa kasi kuwahi kuvuka reli hiyo kabla ya foleni na ndipo lilipolutan na treni hiyo.



ASKARI WAKITAZAMA AJALI HIYO.(PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS)

Akizungumza na mwandishi wa habari, Ofisa Oparesheni Shirika la Reli, Mohamed  Kanka,  alisema kuwa treni hiyo ilikuwa ikipita majira ya saa kumi na mbili alfajiri na kugongwa na gari iliyokuwa ikipita pasipo dereva wa gari hiyo kuzingatia alama iliyokuwa ikionesha kama sehemu hiyo kuna reli.
Alisema kuwa katika ajali hiyo dereva wa gari na dereva aliyekuwa katika treni hiyo wameumia na wamekimbizwa  Hospitali ya Amana Ilala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Vilevile alisema baada ya ajali hiyo kutokea gari jingine lililokuwa limesimama liligongwa na kichwa cha treni baada ya kuiacha njia yake na kuelekea upande wa magari yaliyokuwa yakipita.
Ofisa huyo amewaasa madereva kuwa makini wanapofika eneo lenye alama kuonyesha mbele kuna reli kwani ajali nyingi hutokea kutokana  na madereva wasiokuwa waangalifu.
UMATI WA WATU UKISHUHUDIA AJALI HIYO (PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS)
ENDELA KUPITIA tegeinc.blogspot .com KWA HABARI MBALI MBALI ZA KIUCHUMI,KITAIFA,KIMATAIFA NA BURUDANI.

Wednesday, March 25, 2015

PAZIA LA TUZO ZA MUZIKI ZA KILIMANJARO (KTMA 2015) LAFUNGULIWA RASMI

Msimu mpya wa tuzo za muziki Tanzania zijulikanazo kama Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kwa mwaka 2015 umefunguliwa rasmi.
akizindua msimu huo katika ukumbi wa LAPF uliopo barabara ya ally hassan mwinyi, meneja wa bia ya kilimanjaro bi PAMELA KIKULI alisema “Kilimanjaro Premium Lager ni bia ya watanzania na imejikita katika kuwaletea burudani na pia kutoa majukwaa ambayo yanawapa Watanzania fursa ya kukuza vipaji mbalimbali.. hii tumeithibitisha kwa juhudi za makusudi za kutenga fungu kubwa na kuongeza ushiriki wa wataalaam mbali mbali kwenye fani husika ili kuziendeleza, kuzikuza na kuziongezea thamani tuzo hizi mwaka hadi mwaka sambamba na umaarufu kuongezeka kwenye medani za Kimataifa.”
Bia ya kilimanjaro ambayo ni mdhamini mkuu wa tuzo hizo kwa mwaka huu imedhamini tuzo hizo kwa kiasi cha takribani bil 1.1 za kitanzania kuhakikisha tuzo za mwaka huu zinafanyika kwa ubora na ufanisi wa kimataifa.
Meneja huyo aliongeza kuwa msimu huu hautakuwa na mabadiliko katika vipengele au mfumo wa kuwapata wateule ila kutakuwa na maboresho makubwa katika mfumo wa upigaji kura ili kuongeza ufanisi.

Kura za maoni zitaanza kupigwa tarehe March 30 ambapo shabiki ataweza kupendekeza nani ama nyimbo zipi ziwemo kwenye vipengele vyote vya KTMA 2015.
Watu watapiga kura kupitia mtandao, Whatsapp na SMS na utaratibu uliopo ni kwamba namba moja ya simu itatumika kupiga kura moja kwenye kila kipengele.
Hizi ni njia ambazo utazitumia kupiga kura;
  1. Whatsapp – 0686 528 813.
  2. SMS – 15415.
  3. Mtandao – www.ktma.co.tz
BASATA wamesisitiza usimamizi mzuri wa nyimbo zinazoingizwa; “Kama kuna wimbo ulifungiwa na BASATA hautaruhusiwa kushiriki kwenye mchakato“– BASATA.

Thursday, March 12, 2015

mkono mpya kutoka kwa the starboy nigerian superstar WIZKID. ngoma inaitwa SOUND IT na mzigo umetengenezwa na producer SARZ.
Bonyeza DOWNLOAD kupakua wimbo huu.
kwa hisani ya TEGE INC.

NEW JOINT. KISS DANIEL FT DAVIDO,TIWA SAVAGE - WOJU REMIX. by Tege inc.

mziki wa kiafrika na nigeria unazidi kukua. Na sasa hivi ni zamu ya msanii KISS DANIEL ambaye mwanzoni alitamba na wimbo wake uitwao shoye ambao ulisaidia kumtambulisha vyema kwenye ulimwengu wa muziki nchini nigeria na nchi jirani. Safari hii amekuja na hit song nyengine iitwayo WOJU remix akiwashirikisha Davido na TIWA SAVAGE. Mikono ya DJ COUBLON ndo imehusika kwenye mapishi.
Bonyeza hapa kudownload wimbo huo.  kwa hisani ya tege inc.

Wednesday, March 11, 2015

SOMA HUKUMU WALIYOPEWA PHARELL NA ROBIN THICKLE BAADA YA KUPATWA NA HATIA YA KU- COPY WIMBO BLURRED LINES

Katika zama tunazoishi hususani za tekinolojia inayokua kwa kasi namna hii, masuala ya haki miliki yanaendelea kuwa changamoto ya kidunia. Mfano ni uamuzi wa mahakama huko Los Angeles uliotolewa hivi katika kesi iliyokuwa imefunguliwa na familia ya Marehemu Marvin Gaye ambaye alikuwa miongoni mwa wanamuziki mahiri sana enzi zake.
Familia ilikuwa inawatuhusu wanamuziki Pharrell Williams na Robin Thicke kwamba wimbo wao wa mwaka 2013 uliotamba vilivyo wenye jina “Blurred Lines”, sio wao bali waliiga takribani midundo nk kutoka katika nyimbo ya baba yao ya mwaka 1977 iliyoitwa “Got to Give It Up”.

Katika taarifa ambazo zimeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani, mahakama hiyo imeridhia mashtaka yaliyowasilishwa na kukubali kwamba ni kweli Pharrell na Robin Thicke walifanya “uhuni” na hivyo kuwaagiza wawalipe familia ya Marvin Gaye kiasi cha Dola Za Kimarekani $7.3 (zaidi ya Bil. 126 Tshs). Hata hivyo mwanamuziki mwingine ambaye alishirikishwa katika wimbo huo, T.I mahakama imeona hana hatia yoyote na hivyo hahusiki katika malipo.
Tayari wakili aliyekuwa akiiiwakilisha familia ya Marvin Gaye ameshapeleka maombi ya kusimamisha uuzwaji wowote wa “Blurred Lines”. Hata hivyo kiwango cha Dola Za Kimarekani Milioni $7.3 ni kidogo kulinganisha na kile ilichokuwa inataka kulipwa familia ya Marvin Gaye cha dola milioni $45.

BONYEZA HAPA KUANGALIA JINSI NYIMBO HIZO ZINAVYOSHABIHIANA.

NIYONZIMA AGOMA KUSAINI MKATABA MPYA YANGA

YANGA wajanja sana, kwani wanataka Haruna Niyonzima asaini mkataba mpya na klabu yao halafu malipo yafanyike baadaye kwa awamu jambo ambalo limepingwa na kiungo huyo raia wa Rwanda.
Niyonzima ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao itafikia tamati mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara ifikapo Mei, mwaka huu.Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa kiungo huyo, jamaa huyo amesitisha mazungumzo yoyote kuhusu usajili na Yanga kwani uongozi haukumuonyesha dalili za kumpatia fedha badala ya kumtaka asaini kwanza halafu malipo baadaye.
“Wamemuambia asaini kwanza halafu malipo baadaye, hilo jambo limemuudhi na ameona kama anadharauliwa kwani kwa thamani yake si mtu wa kusaini kwa mali kauli, hivyo sasa anajipanga kutafuta timu nyingine,” alisema rafiki huyo.
Mwandishi wetu alipomtafuta Niyonzima alisema: “Siwezi kusema lolote rafiki yangu kwani ninachojua nimebakiza miezi michache kabla ya mkataba wangu kuisha, baada ya hapo nitakuwa na jibu la kukupa, kwa sasa wacha niitumikie Yanga.”
Hata hivyo, blogu hii inafahamu kuwa Niyonzima yupo katika harakati za kusaka timu mpya kwani haoni dalili za kupewa usajili mpya wa donge nono kwenye kikosi hicho.“Mimi kazi yangu ni mpira, hivyo timu yenye fedha ikinifuata kuzungumza nami nitaisikiliza kuhusu ofa yao japokuwa naipa kipaumbele Yanga kwanza,” alisema Niyonzima.
Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili ya Yanga, Seif Ahmed ‘Seif Magari’, alisema: “Hilo suala muulize mwenyekiti Chanji (Isaac), maana ndiye anajua jinsi ya kukujibu.”
Chanji hakuweza kupatikana kwani simu yake ilikuwa inaita bila kupokelewa na hata Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, hakuweza kupatikana.
Baadhi ya wachezaji wengine wa Yanga wanaomaliza mikataba yao baada ya ligi kuisha ni Mrisho Ngassa, Said Bahanuzi anayecheza kwa mkopo Polisi Moro na Mbuyu Twite.
by TEGE INC BLOG.

AJALI MBAYA YATOKEA MAFINGA MKOANI IRINGA LEO,ZAIDI YA WATU 30 WASADIKIWA KUPOTEZA MAISHA.

Watu zaidi ya 30 wanasadikiwa kupoteza na maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya sana katika ajali mbaya iliyotokea mapema leo asubuhi,maeneo ya Changarawe,Mafinga Mkoani Iringa,iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea baada ya Lori hilo la Mizigo lililokuwa likitokea Jijini Dar kuelekea Mbeya kuligonga na kuliangukia basi hilo wakati lililokuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara wakati wakiwa kwenye mwendo walipokuwa wakipishana. 


Hali ya Uokoaji wa maiti na majeruhi walionasa kwenye ajali hiyo bado ni tete na hasa kutokana na ukosefu wa Gesi ya kukata basi hilo kukosekana eneo lote la Mafinga,Juhudi zinafanyika ili kuweza kuokoa majeruhi pamoja na maiti.

Blog ya tege inc inaendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hili ambalo ni la kusikitisha sana na ni msiba mkubwa kwa taifa,na tutaendelea kujuzana kupitia hapa hapa.
















Blog ya tege inc inatoa pole kwa wahanga wote na wafiwa wote kutokana na ajali iyo. Mungu azipokee na kuzilaza mahala pema peponi roho za marehemu wote katika ajali hii na awajaalie kupona kwa haraka majeruhi wote.

Amin.

BURUDANI YA MAONYESHO YA PIKIPIKI KAWE DAR ES SALAAM

Waendesha Pikipiki wakianza mwendo kwa pamoja wakati wakishindana katika mazoezi yao ya kujiweka fiti kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita. 
 Mwendesha Pikipiki, Ludan Volvo, akiwa hewani baada ya kuruka Tuta, wakati wa mazoezi ya waendesha Pikipiki yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.
Mechi no.117 iliyowakutanisha Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa, imeingiza jumla ya sh. milioni 436,756,000 kutokana na idadi ya watazamaji 49,758 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.

Watazamaji 309 walikata tiketi za VIP A,
1,310 VIP B,
1,533 VIP C,
Rangi ya Machungwa (Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani wakiingia watazamaji 36,693.

Mgawanyo wa mapato ya mchezo huo ni
VAT 18% sh.66,623.796, FDF timu mwenyeji sh. 17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700, Gharama za tiketi sh.11,669,600.

Mgao wa Uwanja sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo sh.28,354,606.29, Bodi ya Ligi (TPLB) sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20, DRFA sh. 11,675,426.12, klabu ya Simba sh. 115,086,343 huku Yanga wakipata sh.81,727.83.

Wakati huo huo Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea kesho siku ya jumanne katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro watawakaribisha Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani.

Siku ya jumatano JKT Ruvu watawakaribisha Young Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya Azam FC.

Aidha mechi ya Kombe la Shirikisho (CC) barani Afrika kati ya Young Africans dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbabwe, itafanyika siku ya jumapili Machi 15, 2015 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

New AUDIO | Makomando - Shake Body | Download/Listen

PAKUA NGOMA MPYA KUTOKA KWA MAKOMANDO


Twitter: @jonnievincy    
Instagram: @jonnievincy    
Facebook Fans Page: jonnie vincy

New AUDIO | GODZILLA - NOBODY | Download/Listen


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgSzDrKKBuaTaQvUs_c3rIw-V-lbKDEJLaDN2EylBZa_w1-llB8b_NTQ_JP8z7uO8vsq1Sxsmk5KPtjWcmF5qF0Opr_6YtN-2lYoX-1WD9a2sCcqyKUvUEWH5Ala6IAv8Siyu2d138Qv4g/s1600/King+Zilla+-+Nobody+artwork.png

https://mkito.com/song/nobody/13430/bwi-1-26911
Click hapa kudownload ngoma mpya kutoka kwa GODZILLAH.

Usisahau kumfollow blogger kupitia twitter: jonnievincy
                                                       facebook : jonnie vincy
                                                       instagram : jonnievincy