Wednesday, April 1, 2015

VIPAJI WILAYA YA KINONDONI SASA KUNG'AMULIWA, KUENDELEZWA.


Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, katika kuhakikisha anainua vipaji ya watoto na vijana  kutoka wilayani mwake ameamua kuanzisha Shindano la Kinondoni Talent Search, ambayo litahusika na kusaka vipaji vya watoto na vijana wenye vipaji vya kucheza, kuimba, kuchekesha na vinginevyo kutoka wilaya kinondoni.
Akizungumza na wakati wa uzinduzi huo, mh Makonda amesema lengo  kubwa la tamasha hilo lenye kauli mbiu ya “Kipaji chako, ajira yako”  litakuwa ni  kuwatafuta na kuwaendeleza vijana wenye vipaji mbalimbali vikiwemo kuimba, kucheza na kuchekesha waliokosa nafasi ya kusikika kutokana na hali ya uchumi kuwa mgumu.
Mh, Paul Makonda akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Kinondoni Talents Search
“Shindano litaanza hivi karibuni, tunataka tuwawezeshe vijana kutoka Wilaya ya Kinondoni waweze kujiajiri kupitia vipaji vyao, na  ili kuhakikisha shindano linaenda vizuri tumeandaa kamati ya watu watano ambao kwa namna moja au nyengine wanatokea kwenye tasnia hiyo ya sanaa wakiwemo Jokate Mwegelo, Mc Pilipili na Peter Msechu,” alisema Makonda,
Msanii Peter Msechu akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.
Akizungumza na waandishi, amesema kuwa Kinondoni Talent Search, ni mpango utakaolenga kuwatambua na kuwaendeleza vijana waishio kwenye wilaya ya Kinondoni, wenye vipaji vya kuimba, kuchekesha na kucheza  ambao wengi wao wapo katika mazingira magumu ya kiuchumi jambo linalowafanya kushindwa kuonesha vipaji vyao.
Amesema kutokana watoto hao wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kuishi katika maisha magumu na kusema kuwa lengo kuu la mpango huu ni kuwawezesha kupata njia za kutimiza ndoto zao kupitia vipaji vyao kwa kuwatafutia nafasi za mafanikio kutokana na ukuaji wa sanaa, kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na wadau muhimu kwenye sekta yao.
Mc pilipili akitoa maelezo wakati wa uzinduzi (picha kwa hisani ya Global publ)
Blogu hii na tasnia ya habari kwa ujumla, inatambua na inampongeza sana mh Paul Makonda kwa hatua nzuri ya kuamua kuendeleza vipaji ambavyo vingi vinapotea sababu ya kukosa wadau wa kuviendeleza. Kwa pamoja tunaunga mkono harakati hizi za ukombozi dhidi ya vijana wenzetu ili kuvifanya vipaji vya vijana wenzetu kuwa ajira itakayotumika kusaidia na kukomboa jamii yote inayotuzunguka. Tunaahidi kuwa nawe bega kwa bega kutimiza jukumu hili zito.
- Tege inc blog -